Psalms 134

Wito Wa Kumsifu Mungu

Wimbo wa kwenda juu.

1 aMsifuni Bwana, ninyi nyote watumishi wa Bwana,
ninyi mnaotumika usiku ndani ya nyumba ya Bwana.
2 bInueni mikono yenu katika pale patakatifu
na kumsifu Bwana.

3 cNaye Bwana, Muumba wa mbingu na dunia,
awabariki kutoka Sayuni.
Copyright information for SwhNEN